
Golikipa mahili wa Mbeya City Fc, Juma K Juma amerejea kikosini kutoa mapumziko ya majuma mawili aliyopewa na kocha Kinnah Phiri kufuatia mkwewe Bi Nasra Nassor kujifungua watoto mapacha hivi karibuni.
Akizungumza na mbeyacityfc.com muda mfupi uliopita Kaseja amesema kuwa amefurahi kusafiri na hatimaye kurudi salama kwenye timu yake huku pia akitoa shukurani zake za dhati wa wale wote ambao wamekuwa karibu nae yeye kama mchezaji na pia familia yake tangu alipojiunga na City.
“Nashukuru mungu nimefika hapa salama baada ya safari yangu, pia namshukuru kwa kile alichonijaalia, nimerudi kikosini nikiwa na ari kubwa zaidi ili kuituikia timu yangu kwa nguvu zote katika kutafuta mafanikio hasa kwenye kipindi hiki ambacho ligi inaelekea mwishoni, hakika tunapita kwenye kipindi kigumu lakini umoja wetu utatufanya kuvuka hapa” alisema.
Akiendelea zaidi Kaseja aliyewahi kucheza kwa mafanikio kwenye timu za Moro United, Simba, na Yanga aliweka wazi kuwa anaimani kuwa na kocha Kinnah Phiri kuwa ataijenga upya City na kuifanya kuwa timu itakayotisha zaidi kwenye msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Post a Comment