
Bondia Nick Blackwell alikimbizwa hospitali baada ya kupigwa na Chris Eubank Jr katika pambano la uzito wa uzani wa kati nchini Uingereza lililofanyika jana Jijini London.
Refa wa pambano hilo alilazimika kulisimamisha katika raundi ya 10, baada ya daktari kushauri Blackwell hatoweza kuendelea kutokana na uvimbe kwenye jicho lake la kushoto.
Bingwa huyo aliyedundwa baadaye alilazimika kuondolewa kwenye ulingo kwa kutumia machela na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Bondia Nick Blackwell akipingwa ngumi ya kushoto na Chris Eubank Jr
Post a Comment