0

Museveni na KenyattaMuda mfupi baada ya Rais Yoweri Museveni kutangazwa mshindiuchaguzi wa urais nchini Uganda, ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta akimpongeza kwa ushindi wake ulipakiwa kwenye kurasa zake Twitter na Facebook.

“Nina furaha sana kumpongeza Mtukufu Rais Yoweri Museveni kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Uganda. Watu wa Uganda wamenena, na wamenena kwa uwazi. Tunaheshimu uamuzi wao wa Rais Museveni.”
Rais Kenyatta alisema Kenya inathamini sana urafiki wa karibu ambao umekuwepo na kwamba anatarajia urafiki huo pamoja na ushirikiano hasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki utaendelea.
“Namtakia Rais Museveni ufanisi anapoendelea kutumikia taifa lake kwa muhula mwingine. Yeye na Uganda wanaweza kutarajia uungaji mkono wangu, na urafiki kutoka kwangu, pamoja na kutoka kwa kaka na dada zao hapa Kenya.”

Post a Comment

 
Top