Umoja wa Mataifa umeelezea hofu kuhusu hali ya taharuki iliyotanda nchini Uganda hususan baada ya uchaguzi mkuu wa urais uliokamilika majuzi
Afisi ya haki za kibinadamu ya Umoja huo inaelezea wasiwasi kufuatia kuwepo kwa hali ya uhasama mkubwa baina ya rais wa jamhuri Yoweri Museveni na viongozi wa upinzani akiwemo kanali mstaafu Kizza Besigye.
Kuimeibuka taharuki kufuatia mauaji ya watu wawili na vilevile kamata kamata ya kiongozi wa upinzani daktari Kizza Besigye kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya urais.
Katika taarifa yake Umoja wa mataifa unaelezea jinsi maafisa wa usalama wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi wanapokabiliana na watu wasiokuwa na silaha ambao msimamo wao unaelekea upande wa chama cha upinzani FDC.

''Inatisha sana ukitizama shime ambayo polisi na jeshi la Uganda ilikuwa nayo ilipovamia afisi za chama cha FDC siku ya ijumaa '' taarifa hiyo inaelezea.
Post a Comment