
Sasa PSG na Real Madrid wanaonyesha kiasi kikubwa wanamtaka mchezaji huyu ajiunge na vikosi vya kwenye ligi zao. Sasa hivi Robert bado yupo kwenye mkataba na Bayern Munich tangu asaini mwaka 2014 akitokea Borussia Dortmund.
Mkataba wake unamfanya akae kwenye club hiyo kwa muda wa miaka 5. Lakini habari mpya ambayo sio nzuri kwa Real Madrid na PSG ni kwamba Lewandowski ameshafungua milango ya kuzungumza kuongeza mkataba na club yake ya sasa.
Baada ya kufunga magoli 31 kwenye mechi 30, sio rahisi club ya Munich kukataa matakwa ya mchezaji huyu ambae amekua mchango mkubwa kwenye mechi zao.
Jumamosi hii Bayern Munich itacheza mechi nyingine ya kwenye ligi ya Bundeslige Vs Hoffenheim. Fuatilia mechi hii kwenye king’amuzi cha Startimes.
Post a Comment