0

samson-siasia






Chama Cha Soka Nchini Nigeria kimemteua Samson Siasia kuwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya Sunday Oliseh kujiuzuru mapema siku ya Alhamisi.
Siasia atakuwa pamoja na wasaidizi wake Emmanuel Amuneke, Salisi Yusuph pamoja na Alloy Agu.
Mabadiliko haya yanafuatia kitendo cha Oliseh kujiuzuru ghafla wiki chache kabla ya Nchi hiyo kukutana na Misri katika michezo ya kufuzu mataifa huru ya Afrika mwaka 2017.
Siasia ambaye ameshawahi kuifundisha timu ya taifa ya Nigeria miaka ya nyuma, ameamuliwa kuingoza Nigeria kushinda michezo yake miwili ijayo dhidi ya Misri mwezi ujao.
Alloy Agu pamoja na Salisu Yusuph walikuwa ni wasaidizi wa Sunday Oliseh lakini wao wamebaki kazini baada ya Oliseh kuamua kujiuzulu.
Emmanuel Amuneke ambaye ni mchezaji wa zamani wa Super Eagles alifanikiwa kukiongoza kikosi cha kizazi cha dhahabu cha under 17 cha Nigeria mwaka 2015 kuchukua kombe la dunia la vijana chini ya umri huo kule nchini Chile.
Chris Green ni mwenyekiti wa benchi la ufundi na kamati ya maendeleo katika chama cha soka nchini Nigeria aliiambia thenff.com hawa tuliowachagua wana jukumu jipya la kuhakikisha wanawafikia wachezaji wa Nigeria popote pale walipo, michezo dhidi ya Misri sio ya kujifurahisha tunahitaji matokeo mazuri kwenye michezo hiyo.
Nigeria wapo katika nafasi ya pili kwenye kundi G la kufuzu fainali za mataifa huru ya Afrika mwaka 2017 wakiwa nyuma ya Misri kwa pointi mbili
Uwanja wa Ahmadu Bello uliopo Kaduna ndiyo utatumika kwenye pambano la Super Eagles na mafarao  kutoka Misri tarehe 25 mwezi ujao.

Post a Comment

 
Top