0







Neymar amepachika goli wakati Barcelona ikishinda kwa mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali wa kwanza ya kombe la Copa del Rey dhidi ya Athletic Bilbao kwenye dimba la San Mames.

Mabigwa hao watetezi wa kombe hilo walicheza bila Lionel Messi aliyepumzishwa pamoja na Luis Suarez anayetumikia adhabu, lakini walipata mabao 2 ndani ya dakika 25 za mwanzo.

Barcelona ilipata goli la kwanza kupitia kwa Munir el Haddadi aliyeunganisha wavuni krosi ya Ivan Rakitic, kabla ya Neymar kufunga bao la pili.

Post a Comment

 
Top