0




















Michuano ya Olimpiki itakayofanyika Rio nchini Brazili inakabiliwa na hofu ya ongezeko la virusi vya Zika vilivyosababisha watoto 4,000 kuzaliwa na vichwa vidogo nchini humo.

Watanzamaji wanawake na wanariadha waliokatika umri wa kupata ujauzito wametahadharishwa na wataalam wa masuala ya afya duniani kufikiria vyema mipango yao ya kwenda Brazili kutokana na hofu ya watoto watakaowazaa kukabiliwa na ugonjwa huo.


Urusi na Australia wameonyesha hofu kwa wanamichezo wanawake wanaojiandaa kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Rio mwezi Agosti, huku mashirika kadhaa ya ndege yakiwapa fursa wanawake wajawazito waliokata tiketi kuhudhuria michuano hiyo kuziuza kwa watu wengine.


Post a Comment

 
Top