0
















Askofu Gilbert Deya ambaye awali alikumbwa na kashfa ya watoto wa miujiza, amehusishwa safari hii na miujiza feki mwingine wa kuwauzia watu mafuta ya mzaituni na kudai kuwa yanatibu Ukimwi.

Askofu huyo ambaye alitimka Kenya na kwenda kuishi Jijini London Uingereza baada tuhuma za kuwateka watoto amenaswa na gazeti moja la Uingereza akiuza chupa za mafuta ya mzaituni za mililita 750 kwa gharama ya shilingi 200 hadi 750 za Kenya.


Mhubiri huyo mtata pamoja na wasaidizi wake wamesema wamekuwa kiuuza mafuta hayo wanayodai kuwa yanatibu Ukimwi, ambayo huyanunua eneo la Aldi, kwenye duka la bidhaa kusini mwa London.

Post a Comment

 
Top